Wanyama Kumfuata Samatta Ubelgiji - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, August 23, 2019

Wanyama Kumfuata Samatta Ubelgiji


Klabu ya Tottenham Hotspur imeripotiwa kuwa katika mazungumzo na Club Brugge ya nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuwauzia kiungo Mkenya Victor Wanayama kwa kiasi kinachotajwa kufikia pauni milioni 11. 

Victor Wanyama


Inaripotiwa Brugge wapo katika mpango wa kutaka kumsajili Wanyama ,28, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Ulaya Septemba 2. 

Spurs walimsajili Wanyama kwa Pauni milioni 11 akiwa kabakiza mkataba wa mwaka mmoja na Southampton mwaka 2016. 

Tottenham wanataka kumuuza kiungo huyo kwa hela ile ile waliyomnunulia ambayo ni Pauni milioni 11. 

No comments: