Azania Benki yatangaza washindi wapya wa promosheni ya 'AMSHA NDOTO' - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, September 5, 2019

Azania Benki yatangaza washindi wapya wa promosheni ya 'AMSHA NDOTO'

Benki ya Azania (ABL) leo imewatangaza washindi wa awamu ya pili ya promosheni yake ya ‘Amsha Ndoto’ ambayo ina lengo la kuwahamasisha wateja wake na umma wa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba itakayowasaidia kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha. 

Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Thobias Samwel (kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanyika kwa droo ya kupata washindi iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Humud Semvua, mjumbe kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha
Promosheni hii ambayo ni ya mizezi mitatu ilianza rasmi tarehe 27/06/2019 na inatarajia kufikia tamati tarehe 27/09/2019 huku ikihusisha wateja wa Azania Benki wa zamani na wale wapya na imejikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti pamoja na Watoto Akaunti. 

Mwezi Agosti, droo ya kwanza ya promosheni hii ilifanyika ambapo jumla ya washindi watatu walipatikana ambao wote kwa pamoja walijishindia jumla ya shilingi millioni 8. 

Akitangaza washindi kwenye droo ya mwezi huu ambayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Thobias Samwel, amesema benki imetimiza ahadi ya kuwapatia zawadi washindi walioshoriki kwenye promosheni na kwamba zawadi wanazopewa zitawasaidia kutimiza ndoto zao. “Katika droo iliyopita tulipata washindi kutoka Arusha, Tunduma paamoja na Dar es Salaam na wote walipewa zawadi zao kama walivyostahili,” amesema Samwel. 

Kwa mujibu wa Samwel, washindi wa mwezi huu wa promosheni hii ambao wamepatikana baada ya droo kufanyika ni; (kiasi cha fedha walichojishindia kwenye mabano); 1. Lucas Brian Temu kutoka Mwanza (Sh milioni 3) 2. Amos Wankara Nyansada kutoka Geita (Sh milioni 3) 3. Alye Awadhi kutoka Geita (Sh milioni 2) 

Huku ukiwa umebaki mwezi mmoja kampeni hii kufika tamati, Samwel amesema kuwa ili mtu aweze kushiriki kwenye promosheni ya Amsha Ndoto ni lazima kwanza awe mteja wa Azania Benki mwenye akiba ya kiasi kisichopungua TZS 1,000,000 ambaye anapewa tokeni zinazomwezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho inayowapata washindi. Wanaobahatika kushinda watafurahia riba ya 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima. 

Akitoa pongezi kwa washindi wa promosheni, Samwel amewahasa wateja wa ABL kushiriki kwa wingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo inayofuata huku wakijahakikishia kuwa na akiba ya kutosha kwenye akaunti zao kwa ajili ya matumizi yao ya siku za usoni. 

Kwa mujibu wa Samwel, ‘Ziada Akaunti’ ni kwa ajili ya watu binafsi na wafanyabiashara wadogo (SMEs) wanaotaka kujivuna kiwango kizuri cha riba. Mmiliki anaweza kuweka akiba muda wowote na kuweza kutoa kila baada ya miezi mitatu. Na ‘Watoto Akaunti’ ni kwa ajili ya watoto, akaunti ambayo inafunguliwa na mzazi kwa ajili kumwekea akiba mtoto wake. 

“Tunawahamasisha wazazi wote na walezi kuwafungulia Watoto wao ‘Watoto Akaunti’ ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye kwani akaunti hii inaweka msingi wa kuwaandaa watoto kujifunza namna ya kuweka akiba kuanzia kwenye umri mdogo”, amesema Samwel. 

No comments: