Bilionea Jack Ma Atangaza Kustaafu Kuiongoza Kampuni Ya Alibaba Akisherehekea kutimiza Miaka 55 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, September 10, 2019

Bilionea Jack Ma Atangaza Kustaafu Kuiongoza Kampuni Ya Alibaba Akisherehekea kutimiza Miaka 55

Bilionea huyo aliyechoche biashara kupitia mtandao (Internet) ameondoka rasmi katika nafasi ya Mwenyekiti Mkuu wa Kampuni ya Alibaba. Hatua hii ya Jack Ma, inakuja ikiwa ni baada ya muongo mmoja wa kuijenga kampuni hiyo hadi kufikisha kiasi cha Dola Bilioni 460 katika mzunguko wake wa biashara

Katika sherehe yake ya kutimiza miaka 55 Jack Ma amesema anataka kujaribu kufanya mambo mapya katika sekta nyingine kabla hajafikisha miaka 70. 

Kampuni ya Alibaba inajihusisha na kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao (Online) na ilianzishwa Aprili 4, 1999 kwa ushirikiano wa Jack Ma na Peng Lei. 

No comments: