Madeni Yazidi Kumuandama Birdman, Sasa Atakiwa Kumlipa Mfanyakazi wake Mabilioni - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, September 13, 2019

Madeni Yazidi Kumuandama Birdman, Sasa Atakiwa Kumlipa Mfanyakazi wake Mabilioni


Birdman ananuka madeni tu, kila uchwao yanaibuka mapya kuhusu watu ambao wanamdai. Leo kuna hii mpya ya mfanyakazi wake ambaye alimshtaki kwa kushindwa kumlipa mshahara.Mtandao wa The Blast umeripoti kuwa Mahakama imemtaka Birdman kumlipa mfanyakazi huyo kiasi cha ($1M) sawa na Bilioni 2.2 za Kitanzania kama fidia kwa kesi yao ya mwaka 2018 ambayo jamaa huyo Nicolas Jose Penzo alimburuza Birdman pamoja na Cash Money kwa kushindwa kumlipa mshahara.

Penzo alikuwa anamdai Boss huyo wa Cash Money Tsh. Milioni 47 lakini kutokana usumbufu aliamua kufungua shtaka jipya na kutaka alipwe Bilioni 2.2 - Birdman ameshindwa kufika mahakamani na Penzo amepewa ushindi wa kesi hiyo. 


No comments: