Mawakala Shirika La Ndege Tanzania Wahukumiwa Kwa Kulisababishia Hasara Shirika Hilo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, September 4, 2019

Mawakala Shirika La Ndege Tanzania Wahukumiwa Kwa Kulisababishia Hasara Shirika Hilo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu mawakala 12 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kulipa faini ya sh.Millioni moja kila mmoja ama kwenda jela miaka 20 baada ya kukiri kosa la kulisababishia Shirika hilo hasara ya zaidi ya Sh. Milioni kumi.Pia washtakiwa hao wote wameamriwa kulipa fidia ya Sh 10,874,280 na mahakama pia imeamuru zana ambazo walizitumia katika kusababisha hasara ambazo ni simu kumi na tatu na Laptop sita zitaifishwe na kuwa mali ya serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Akisoma Hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally amesema amezingatia hoja zilizotolewa na pande zote mbili, ule wa mashtaka na Utetezi baada ya washtakiwa hao kukiri makosa yao.

Washtakiwa hao waliohukumiwa ni Fabian Ishengoma, Adamu Kamara, Marlon Masubo, Alexander Malongo, Tunu Kiluvya, Jobu Mkumbwa, Mohamed Issa, Godfrey Mgomela, Absalom Nyusi na Janeth Lubega. Mary semakweli Janet Lubega.

Mapema kabla ya kusomwa kwa adhabu Hakimu Ally aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na chochote cha kusema, ambapo wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao na kwa wengine wenye tabia kama hiyo. Pia aliiomba mahakama iamuru laptop na simu za mkononi zilizotumika katika kuisababishia serikali hasara zitaifishwe na kuwa mali ya serikali. Aidha aliiomba mahakama washtakiwa hao kulipa fidia ya hasara waliyoisababishia ATCL.

Katika utetezi kwa niaba ya washtakiwa, Wakili Benedict Inshabakaki amedai washtakiwa hao ni wakosaji wa kwanza na kwa kuwa wamekiri mashtaka yao wenyewe tunaomba wapunguziwe adhabu kwa kuwa awajaisumbua mahakama na vile vile ni vijana wadogo ambao wanafamilia zinazowategemea na pia ni nguvu kazi ya kesho.

Wakili Inshababakaki ameendelea kudai kuwa, Wateja wake hao wamekaa ndani kwa zaidi ya miezi nane, hivyo watakuwa wamejifunza na wanajutia hivyo, tunaomba walipe faini na siyo kifungo gerezani.

"Licha ya washtakiwa kuonesha kujutia kitendo hicho cha kuisababishia ATCL hasara natoa adhabu ya kila mshtakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni moja ama kwenda jela miaka 20, pia wanatakiwa kulipa fidia ya hasara hiyo kwa ATCL mahakama pia inaamuru zana zilizotumika katika kusababisha hasara ambazo ni Simu 13 na Laptop sita zitaifishwe kuwa Mali ya serikali na kama washtakiwa hamjaridhika na hukumu, rufaa iko wazi" amesema Hakimu Ally.

Katika keai hiyo washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh10,874,280.

No comments: