Mtandao Wa Facebook Wadukuliwa, Taarifa Za Akaunti Milioni 210 Zavuja - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, September 10, 2019

Mtandao Wa Facebook Wadukuliwa, Taarifa Za Akaunti Milioni 210 Zavuja

Jumla ya data zilizowekwa wazi zinaonesha ni data zinazohusisha akaunti milioni 419 ila Msemaji wa Facebook amesema baada ya kuzipitia wamegundua ni milioni 210 huku akidai data hizo nyingi ni za akaunti za zamani na nyingine zimerudiwaData hizo zimehusisha taarifa muhimu kuhusu watumiaji wa Facebook kama vile anuani za akaunti zao, namba zao za simu na pia kwa baadhi ni majina yote ya muhusika

Data hizo zimehusisha watumiaji wa Marekani zaidi ambapo akaunti milioni 133 kati ya 210 zilikuwa za watumiaji wa nchi hiyo

Akaunti milioni 50 zikiwa za watumiaji kutoka Vietenam, milioni 18 zikiwa za Waingereza na kupelekea udukuzi huu kuchukua sifa ya kuwa moja ya udukuzi mkubwa zaidi wa data duniani kwa idadi ya watumiaji

Udukuzi huu umekuja wakati mbaya kwani tayari Facebook wanapata pingamizi kutoka Bunge la Marekani (Congress) kuhusu wazo la kuja na sarafu yao ya kidigitali – Libra

No comments: