Papa Francis Kuanza Ziara Katika Nchi Za Afrika Leo Jumatano - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, September 4, 2019

Papa Francis Kuanza Ziara Katika Nchi Za Afrika Leo Jumatano

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis leo Jumatano anaanza ziara ya wiki moja, akitembelea nchi za Afrika ambazo zimekumbwa na umaskini, vita pamoja na majanga ya asili. Papa Francis atatembelea Msumbiji, Madagascar pamoja na Mauritius, nchi ambazo zilitembelewa na papa John Paul II mwaka 1988 na 1999. 

Wachambuzi wanaona uamuzi huo wa papa kutembelea nchi mbili kati ya nchini maskini kuliko zote duniani, kuwa ni kitendo cha mshikamano kutoka kwa kiongozi ambaye mara kwa mara amekuwa kwenye vitongoji maskini nchini Argentina. 

Msumbiji ni ya kwanza katika ziara yake, na ujumbe wa papa uliorekodiwa kwa lugha ya Kireno kabla ya ziara yake, unataja ziara ya Papa John Paul. 

Lakini mtu anayejulikana kama "papa wa maskini" ataweza kutembelea miji mitatu tu mikuu ya nchi hizo. 

Uamuzi huo hautawafurahisha wananchi wa jiji la Beira ambao uko katikati ya Msumbiji, ambako kimbunga kinachoitwa Idai kiliua watu wasiopungua 600 na kuacha maelfu wakiwa hawana makazi mwezi Machi. 


No comments: