Rafael Nadal Bingwa Mpya US OPEN 2019


Mhispania Rafael Nadal ameshinda ubingwa wa Tennis wa mashindano ya 'US Open 2019' baada ya kumfunga Mrusi Daniil Medvedev kwa seti 7–5, 6–3, 5–7, 4–6, 6–4 katika mchezo wa fainali hapo jana. Nadal (33) sasa ameshinda ubingwa wa US Open kwa mara ya 4 na hii ni Grand Slam yake ya 19 kuchukua, moja nyuma ya Roger Federer mwenye 20. Post a Comment

0 Comments