Serikali Yaagiza Vibali Vya Biashara Ya Vyuma Chakavu Kufutwa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, September 5, 2019

Serikali Yaagiza Vibali Vya Biashara Ya Vyuma Chakavu Kufutwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene amemuagiza Katibu Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC kufuta vibali vyote vya zamani vya wafanyabiashara wa vyuma chakavu. Simbachawene amesema kuundwe tume ambayo itasimamia utengenezaji wa vibali vipya vitakavyokidhi matakwa ya kibiashara. 

Ametoa agizo hilo jana Septemba 4, jijini Dar es salaam wakati akiongea na wafanyabiashara wa Vyuma chakavu ambapo amesema vibali vyote vilivyotolewa awali vimefutwa na utaratibu wa kuboresha vibali hivyo utafanyika upya ndani ya siku Saba. 

“Kamati iundwe ndani ya masaa 24 na iweze kufanya kazi kwa siku saba kukamilisha hivyo vibali vipya, Nemc muwasikilize wafanyabiashara na kuzingatia ukusanyaji wa tozo ili kukuza uchumi wa nchi.”amesema. 

No comments: