SONGAS yalipa Gawio la Tsh Bilioni 8.8 Kwa Taasisi Za Serikali - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, September 6, 2019

SONGAS yalipa Gawio la Tsh Bilioni 8.8 Kwa Taasisi Za Serikali

Kampuni inayojishughulisha na uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati ya gesi SONGAS, jana imetangaza kuilipa serikali ya Tanzania Tsh Bilioni 8.8 kama gawio la hisa zake katika kampuni hiyo. 

Bw Nigel Whittaker, Mkurugenzi Mtendaji Songas Limited (katikati) akitoa taarifa ya gawio mbele ya waandishi wa habari mapema hapo jana. 
Katika Mkutano na waandishi wa habari, Afisa mkuu wa Fedha wa Songas Limited, Bw Anael Samwel amesema kuwa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) litapokea Tsh Bilioni 2.2 huku TPDC ikipokea Tsh Bilioni 6.6 na kuongeza kuwa kiasi hicho kimetokana na uwiano wa hisa zinazomilikiwa na taasisi hizo kwenye kampuni ya Songas. 

Afisa mkuu wa Fedha wa Songas Limited
Afisa mkuu wa Fedha wa Songas Limited, Bw Anael Samwel
"Tangu mwaka 2004, Songas imekuwa ikiwezesha dhamira ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa viwanda kwa kuchangia takribani 20% ya nishati ya uhakika na kwa bei nafuu katika gridi ya taifa, huku ikiendelea kusambaza gesi asilia katika viwanda mbalimbali jijini Dar es Salaam." alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SOngas Limited, Bw Nigel Whittaker 

Mkurugenzi Mtendaji Songas Limited
Bw Nigel Whittaker, Mkurugenzi Mtendaji Songas Limited

Pia katika kumalizia Bw Nigel Whittaker aliongeza kuwa Songas ina mpango wa kuongeza uzalishaji kutoka 180MW mpaka 250MW ili kufikia mahitaji ya Nishati yanayokuwa kwa kasi sana na kuchangia katika sera ya ukuaji wa viwanda nchini. 


No comments: