Takribani Viongozi 10 Wa Afrika Kuhudhuria Mazishi Ya Mugabe Zimbabwe - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, September 13, 2019

Takribani Viongozi 10 Wa Afrika Kuhudhuria Mazishi Ya Mugabe Zimbabwe

Viongozi 10 wa kiafrika wanatarajiwa kuhudhuria shughuli ya maziko ya Rais wa kwanza Zimbabwe Robert Mugabe. Hayo yameelezwa na msemaji mkuu wa Serikali ya nchi hiyo na kuongezea kuwa Mwili wa marehemu ulirudishwa Zimbabwe siku ya Jumatano ukitokea nchini Singapore alikofariki akiwa na umri wa miaka 95. 

Miongoni mwa viongozi wa Afrika waliothibitisha kushiriki katika shughuli hiyo ni pamoja na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Uhuru Kenyatta wa Kenya, na Filipe Nyusi wa Msumbiji. 

Marais wastaafu watakaoshiriki ni pamoja na Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Kenneth Kaunda wa Zambia na Sam Nujoma wa Namibia. 

Serikali ya Zimbabwe imesema Mugabe atazikwa katika makaburi ya kijiji cha Kutama, kiasi kilomita 85 kutoka mji mkuu Harare. 

Msemaji wa familia ya Mugabe pia amesema maziko yatafanyika wiki ijayo jumatatu au Jumanne. 

No comments: