Tetesi na Habari za Michezo Barani Ulaya Leo 12/09/2019 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, September 12, 2019

Tetesi na Habari za Michezo Barani Ulaya Leo 12/09/2019

Klabu ya Real Madrid inaijaribu Liverpool kwa kuwaomba iwauzie beki wao Virgil van Dijk katika kipindi hiki ambacho mchezaji huyo anafanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya pale Anfield. (Source: Daily Express). Klabu ya Valencia wamethibitisha kumfukuza kazi kocha wao Marcelino Garcia baada ya mwanzo mbaya wa msimu huu mpya ndani ya La Liga. Marcelino mwenye umri wa miaka 54 alitwaa taji la Copa del Rey na kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita baada ya kuwa madarakani kwa miaka miwili. 

David De Gea anakaribia kukubali mkataba mpya wa kuendelea kukipiga Manchester United kwa £290k kwa wiki. (Source: Guardian)

“Tulikuwa tunataka kumsajili Lewandowski kwa miaka kadhaa na hakuna kilichotokea kwasababu hakuwa na kipengele cha ada na hawakutaka kumuuza “ - Florentino Perez, Rais wa Real Madrid 

Kiungo wa kituruki Arda Turan amekumbana na wakati mgumu baada ya Mahakama kumuhukumu miaka miwili na miezi 8 kwenda jela kwa kukutwa na hatia kwa kosa la kupiga risasi hospitali na kusababisha paniki na kumilika silaha kinyume cha sheria. 

Arsene Wenger anasema moja ya majuto yake makubwa akiwa kocha wa Arsenal ni kushindwa kumsajili Lionel Messi kutoka Barcelona. Arsenal ilijaribu kumsajili Lionel Messi mwaka 2003 na kushindwa kuipata saini yake. Kipindi hicho ndipo walimsajili Cesc Fabregas. 

Manchester United wapo kwenye mazungumzo na Jesse Lingard juu ya kusaini mkataba mpya. (Source: Daily Star) ‬
No comments: