Tetesi na Habari za Soka Barani Ulaya leo 13/09/2019 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, September 13, 2019

Tetesi na Habari za Soka Barani Ulaya leo 13/09/2019

Gazeti la Tuttosport la nchini Italia linaripoti kuwa Timu za Juventus na Tottenham Hotspurs ziko katika mazungumzo ya awali kuhusu uwezekano wa kubadilishana wachezaji Paulo Dybala kwa Eriksen katika dirisha dogo la usajili la Januari. Mshambuliaji Wilfred Zaha amemwambia wakala wake kuwa yuko tayari kuvunja mkataba wake na klabu ya Crystal Palace baada ya harakati zake za kuondoka klabuni hapo katika dirisha kubwa kukwama. 

Kwa mara ya kwanza Lionel Messi afunguka kuhusu sakata la uhamisho wa Neymar uliokwama kipindi cha dirisha kubwa la usajili. "Sijajua kama Barcelona ilijaribu kwa kila hali kumrudisha Neymar katika dirisha hili au la... Lakini ninachojua ni kuwa Neymar alikuwa anaomba uhamisho huo ukamilike" Alisema Messi alipokuwa akihojiwa na kituo cha SPORT. 

Gwiji wa zamani wa West Ham, Paolo Di Canio amerusha dongo kwa PSG na Mauro Icardi kwa kusema "Alikuwa hapendi kuwapongeza wachezaji wenzake Kama yeye hajafunga katika mechi... Sishangai Icardi kutua PSG... PSG ni sehemu pendwa kwa wachezaji wasio na nidhamu". 

RASMI: Mapema leo hii kinda wa klabu ya Arsenal, Joe Willock amesaini mkataba mpya utakaombakisha klabuni hapo hadi mwaka 2022. 

Kiungo Mcroatia Luka Modric anaongeza idadi ya majeruhi ndani ya klabu ya Real Madrid baada ya kupata majeraha ya nyama za paja akiwa na timu yake ya taifa ya Croatia katika mechi za kufuzu Euro 2020. 


No comments: