Watu 41 Wakamatwa Kwa Kupora Na Kuchoma Moto Maduka Ya Wageni Afrika Kusini - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, September 3, 2019

Watu 41 Wakamatwa Kwa Kupora Na Kuchoma Moto Maduka Ya Wageni Afrika Kusini

Polisi wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waporaji. Mamia ya watu wamekuwa wakionekana wakikimbia na kupora mali za watu katika eneo lenye shughuli za kibiashara na kuchoma moto maduka yanayoaminiwa kumilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika. Ghasia hizo zilianzia katika eneo la Jeppestown, lililopo katika wilaya ya kati yenye shughuli za biashara. Lakini zilisambaa hadi kwenye maeneo mengine kama vile Denver, Malvern, Turffontein, Tembisa na maeneo mengine ya vitongoji. 

Watu 41 wamekamatwa katika wimbi hilo la ghasia. Video iliyosambazwa kwa kiasi kikubwa kwneye mitandao ya kijamii inayoonyesha magari kadhaa yaliyoungua kwa moto katika kile kinachoonekana kama mahala panapoegeshwa magari makuu kuu. 

Polisi wamefyatua mabomu ya kutoa machozi , na risasi za plastiki kujaribu kusitisha uporaji.Msemaji wa polisi Kapteni Mavela Masondo amesema kuwa maafisa wa polisi wamekuwa wakikabiliana na moto katka jengo lililotekwa mjini Jeppestown Jumapili. 

Amesema kuwa watu 3 walikufa katika moto huo, huku mtu wa nne akipata matibabu baada ya kuvuta hewa ya moshi. 

"Wakati bado tunafanya uchunguzi na huduma za dharura , watu waliokuwepo karibu walianza kutumia fursa ya hali iliyopo na kupora maduka." 

Luteni Generali Alias Mawela ambaye ni kamanda wa polisi wa jimbo amesema kuwa polisi wamewakamata walau watu katika kile alichokielezea kama ghasia kubwa. Haijabainika ni akina nani walioanzisha mashambulio hayo. 

Waziri wa polisi Bheki Cele aliyetembelea eneo la ghasia amelaani ghasia hizo ambazo amesema hazina maana. 

"Wakati bado tunafanya uchunguzi na huduma za dharura , watu waliokuwepo karibu walianza kutumia fursa ya hali iliyopo na kupora maduka." 

Baadhi yawatumiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo wamekuwa wakishirikishana picha na video za ghasia hizo. 

Awali aliashiria kuwa kuna kikundi kikubwa cha watu kinachoelekea katikati mwa jiji na wanasomba kila wanakiona njiani:

Wengi miongoni mwa watu 41 waliokamatwa walipatikana na mali walizopora wakiwa wamezibeba mapema jumatatu alfajiri.

Washukiwa wanane walikamatwa ndani ya duka moja.

Kamishna wa polisi wa jimbo la Gauteng Luteni Generali Elias Mawela alielezea matukio haya kama ya ''ukiukaji wa sheria'' na ''yasiyo ya kibinadamu''

"Ni siku ya huzuni wakati watu wanapoamua kutumia matatizo ya wengine kwa ajili ya kuendeleza ukiukaji wa sheria au uhalifu. 


No comments: