Yanga Kuipeleka KUBWA KULIKO Mkoani Mwanza - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, September 4, 2019

Yanga Kuipeleka KUBWA KULIKO Mkoani Mwanza

Uongozi wa klabu ya Yanga umepanga kufanya Tamasha la 'kubwa kuliko' jijini Mwanza keshokutwa Septemba 6 katika uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya kuchangisha fedha ili kusaidia gharama za timu hiyo. Kwa mara ya kwanza Tamasha la kubwa kuliko lilifanyika Juni 16 jijini Dar es Salaam ambapo Yanga ilikusanya zaidi ya milioni 900 kutoka kwa wadau mbalimbali wa klabu hiyo. 

Kaimu Katibu mkuu wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema baada ya Tamasha hilo siku inayofuata walikuwa wacheze mechi ya kirafiki dhidi ya Mbao FC lakini mchezo huo hautafanyika isipokuwa watacheza na Pamba FC. 

Baada ya mchezo huo Septemba 9 watacheza mechi nyingine ya kirafiki ambayo bado haijathibitishwa huku wakiwa kwenye mazungumzo na Gwambina FC kwa ajili ya mchezo huo. "Tutafanya Tamasha la kubwa kuliko jijini Mwanza kama ilivyokuwa hapa Dar es Salaam na tutacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Pamba FC," alisema Ten. 

Kikosi cha timu ya Yanga kitasafiri kesho kuelekea Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa hatua ya kwanza wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Zesco utakaofanyika Septemba 14 katika uwanja wa Taifa. 

No comments: