AKIMBILIA MAFICHONI BAADA YA KUTUHUMIWA KUMBAKA MJUKUU WAKE


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, linamtafuta Hamdu Othman Mcha (65) mwenye wajukuu zaidi ya 20 akituhumiwa kwa kosa la kumbaka mjukuu wake, na kisha kutokomea kusikojulikana

Babu huyo baada ya kudaiwa kufanya kosa hilo, ameitelekeza familia yake kwa muda wa wiki mbili sasa baada ya taarifa za ubakaji kuripotiwa kituo cha Polisi Mtambile

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Hassan Nassir Ali, alisema awali walipokea taarifa kutoka kwa mtoto wa babu huyo akilalamikia babaye kutoonekana lakini uchunguzi umebaini kumbe ameukimbia mkono wa sheria kutokana na tuhuma za ubakaji dhidi ya mjukuu wake.

Post a Comment

0 Comments