Azania Benki yatangaza washindi wa mwisho wa promosheni ya ‘Amsha Ndoto’

Meneja wa mauzo ya rejareja wa Azania Bank Limited, Jackson Lohay  (katikati) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuwatangaza washindi wa promosheni ya Amsha Ndoto iliyoendeshwa na benki hiyo kwa lengo la kuwahamasisha wateja wake kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba.Dar-es-salaam, 4 Novemba 2019: Benki ya Azania (ABL) leo imewatangaza washindi wa awamu ya tatu na ya mwisho wa promosheni yake ya ‘Amsha Ndoto’ ambayo ina lengo la kuwahamasisha wateja wake na umma wa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba itakayowasaidia kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha. 
Promosheni hii ambayo ni ya mizezi mitatu ilianza rasmi tarehe 27/06/2019 na ilifika tamati tarehe 27/09/2019 huku ikihusisha wateja wa Azania Benki wa zamani na wale wapya na ilijikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti pamoja na Watoto Akaunti. 
Mwezi Agosti, droo ya kwanza ya promosheni hii ilifanyika ambapo jumla ya washindi watatu walipatikana ambao wote kwa pamoja walijishindia jumla ya shilingi millioni 8. Vivyo hivyo, droo iliyofuata ilifanyika mwezi Septemba ambapo pia washindi watatu walipatikana wakijishindia jumla ya kiasi cha shilingi milioni 8. 
Akitangaza washindi kwenye droo ya tatu na ya mwisho ambayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Jackson Lohay, amesema benki imetimiza ahadi ya kuwapatia zawadi washindi walioshoriki kwenye promosheni na kwamba zawadi wanazopewa zinawasaidia kutimiza ndoto zao. “Katika droo mbili zilizopita tulipata washindi kutoka Amaeneo mbalimbali ya nchi yetu ya Tanzaniana wote walipewa zawadi zao kama walivyostahili, kwa ujumla washidni wote sita waliweza kujishindia kiasi cha shilingi milioni 16,” amesema Lohay. 
Kwa mujibu wa Lohay, washindi wa droo ya mwisho ya promosheni hii ambao wamepatikana baada ya droo kufanyika ni; (kiasi cha fedha walichojishindia kwenye mabano); 
1. Frank Godfrey Nyange (Tsh2.2m) 
2. Anna Said Lyimo (Tsh 3m) 
3. Venancy Benny Loshia (Tsh 3m) 

Akitoa pongezi kwa washindi wa promosheni, Lohay amewahasa wateja wa ABL kuendelea na utamaduni wa kujiwekea akiba kwani kwa kufanya hivyo wanakuwa wanajihakikishia kuwa na fedha za kutosha kwenye akaunti zao kwa ajili ya matumizi yao ya siku za usoni. Page 2 of

Kwa mujibu wa Lohay, ‘Ziada Akaunti’ ni kwa ajili ya watu binafsi na wafanyabiashara wadogo (SMEs) wanaotaka kujivunia kiwango kizuri cha riba. Mmiliki anaweza kuweka akiba muda wowote na kuweza kutoa kila baada ya miezi mitatu. Na ‘Watoto Akaunti’ ni kwa ajili ya watoto, akaunti ambayo inafunguliwa na mzazi kwa ajili kumwekea akiba mtoto wake. 
“Tunawahamasisha wazazi wote na walezi kuendelea kuwafungulia watoto wao ‘Watoto Akaunti’ ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye kwani akaunti hii inaweka msingi wa kuwaandaa watoto kujifunza namna ya kuweka akiba kuanzia kwenye umri mdogo”, amesema Lohay. 
Kwa mujibu wa Lohay, promosheni ya Amsha Ndoto ilihusisha wateja wa Azania Benki wenye akiba ya kiasi kisichopungua shilingi 1,000,000/- ambao walikuwa wanapewa tokeni zinazowawezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho inayowapata washindi watatu kila mwezi. Wanaobahatika kushinda wamefurahia riba ya 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima. 
Promosheni hii, iliyokuwa na kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde Tumuwezeshe Ada ya Shule’, iliwasilishwa kupitia mitandao ya kijamii na tovuti za ndani za benki. Benki pia ilitengeneza tovuti ndogo, maalumu kwa wateja wapya kujiunga (amshandoto.com). 

Post a Comment

0 Comments