EMINEM Aongelea Wimbo Wake Uliovuja ambao Ndani Kamponda RIHANNA

Eminem amefunguka kuhusu sakata la wimbo wake 'Things Get Worse' kuvuja hivi karibuni, wimbo ambao ndani alikaa upande wa Chris Brown na kum-diss Rihanna baada ya kushushiwa kipigo kizito mwaka 2009."Of course I side with Chris Brown, I'd beat a bitch down too" ali-rap kwamba anakaa upande wa Breezy na hata angekuwa yeye angempa kichapo tu.

Sasa kwenye mahojiano na Gazeti la The Guardian, msemaji wa Eminem, Dennis Dennehy amezungumza kwamba "Huu ni wimbo wa miaka 10 iliyopita, baada ya Eminem kuurekodi, aliutupilia mbali na kuuandika upya. Hata hivyo yeye [Eminem] na Rihanna wana mahusiano mazuri." amesema Dennis.

Wimbo huo ulirekodiwa miezi michache tu baada ya Chris Brown kushtakiwa kwa kosa la kumshambulia Rihanna, lakini baadaye walishirikiana kwenye kubwa za dunia kama "Love The Way You Lie" (2010) pia "The Monster" ya mwaka 2013.

Post a Comment

0 Comments