KIM Kardashian Afunguka Kuhusu Kenya WEST Kuokoka...Adai Amekuwa Mkali..Kaondoa Television Zote Ndani


Kim Kardashian ameeleza mambo mengi ambayo mume wake Kanye West anayafanya kwa sasa baada ya Kuokoka. Amesema malezi yake kwa watoto yamebadilika sana kulinganisha na awali.Kwenye episode mpya ya kipindi cha The Real, Kim amesema Kanye amekuwa muangalifu na mchukua tahadhari mkubwa ndani ya familia yao ikiwemo kuondoa televisheni zote ndani ya vyumba vya watoto. Pia ameongeza ukali kwenye malezi na kupunguza vitendo vya mahaba wao wawili mbele ya watoto.

Post a Comment

0 Comments