KIONGOZI WA KIKUNDI CHA WAASI CHA KABILA LA WAHUTU AUAWA CONGO DR

Vikosi vya Wanajeshi wa Serikali ya Congo vimemuua Musabyimana Juvenal pamoja na walinzi wake wanne baada kuendesha oparesheni katika mpaka wa nchi hiyo na UgandaKulikuwa na matukio kadhaa ya kurushiana risasi katika eneo la Rutshuru lililopo Kivu ya Kaskazini. Oparesheni hiyo ililenga kuondoa vikundi vya Waasi kutoka nchi jirani

Juvenal ni mpiganaji wa kikundi cha Kabila la Wahutu cha Hutu Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) kilichoanzishwa mwaka 1994 baada ya mauaji ya kimbari

Juvenal ameuawa ikiwa ni miezi 2 baada ya Kamanda mwingine wa FDLR, Sylvester Mudacumura kuuawa mnamo Septemba mwaka huu (2019)

Viongozi hao wa Kikundi cha FDRL walikuwa wakisakwa na taasisi za Kimataifa ili washtakiwe kwa makosa mbalimbali

Post a Comment

0 Comments