KOCHA SIMBA AJA NA TAMKO LINGINE JUU YA LIGI KUU BARA


Wakati kikosi chake kikiwa kinaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema anafurahia kuona ushindani uliopo katika ligi hiyo msimu huu umeongezea na kueleza kuwa hali hiyo inaongeza umakini kwenye timu yake.

Aussems alisema ushindani pia unasaidia kuimarisha viwango vya wachezaji kwa sababu kila mmoja anajiimarisha ili apate namba katika kikosi cha kwanza.

Aussems alisema ushindani unapokuwa mkubwa, kila timu inalazimika kuongeza mbinu za kusaka
ushindi kwa sababu hakuna anayeamini atapata matokeo mazuri kabla ya kuingia uwanjani.

"Ushindani ni mzuri, utafanya kila mmoja afahamu hayuko mahali salama, hakuna jambo jepesi,
tunajiimarisha kila siku, kwa sababu tunataka kupata matokeo mazuri, hakuna mechi nyepesi,
hakuna mwenye uhakika wa kushinda nyumbani au ugenini," alisema Aussems.

Mbelgiji huyo aliongeza kuwa mbali na ushindani katika ligi, pia katika kila timu kuna ushindani na
hali hii inasaidia kuwafanya wachezaji "waamke" na kujipanga kupambana.

"Mechi ni ngumu, timu zimeimarika, kila upande sasa unafanya vizuri, tayari wachezaji wameimarika tofauti na tulivyoanza msimu, ili tufikie malengo, tunatakiwa kujituma zaidi," alisema kocha huyo.

Alisema kuwa baada ya kuwapa mapumziko wa siku mbili, kikosi chake kilianza mazoezi ya
kujiandaa na mechi dhidi ya Ruvu Shooting, na anaamini ataendelea kuwatumia wachezaji wote
waliosajiliwa kulingana na aina mpinzani wanayekutana naye.
Post a Comment

0 Comments