Nape Nnauye adai viongozi hawa wanatishiwa


Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema uhaba wa magunia kwa ajili ya kuhifadhi korosho umewafanya viongozi wa ushirika kutishiwa maisha na wengine kufungiwa kwenye ofisi.

“Tangu msimu umeanza (wa korosho) upatikanaji wa magunia ni mbaya sana. Leo asubuhi viongozi wa vyama vya ushirika wanatishiwa maisha wengine wanafungiwa kwenye ofisi.”

“Wakulima wanapatiwa magunia mawili.  Serikali inatoa tamko gani kuokoa hali hiyo,” amehoji Nape bungeni mjini Dodoma leo Bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza.

Akijibu swali hilo naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba amesema kuna changamoto  ya magunia na Serikali imeona.

“Wenye jukumu la kuagiza magunia ni vyama vya ushirika, hao ndio waliagiza lakini baada ya kusuasua tumeingilia kati na kuongea na msambazaji,” amesema.

Post a Comment

0 Comments