Nicki Minaj Hakubaliani Na Swala La Mtandao Wa Instagram Kuondoa 'Likes', Atishia Kujitoa

Nicki Minaj atangaza kuikacha instagram baada ya CEO wa mtandao huo Adam Mosseri kutoa taarifa kwamba wataondoa uwezo wa mtumiaji kuona LIKES kwenye post yake kuanzia wiki ijayo.Nicki Minaj alienda kwenye insta stories yake na kueleza kwamba instagram wameamua kufanya hivyo ili kuwanyima madili watu wenye ushawishi mkubwa ambao walikuwa wanategemea kuonesha idadi ya LIKES ili kupata matangazo mbali mbali. Alienda mbali zaidi na kusema wanataka watu wote waanze sasa rasmi kuwalipa instagram kwa kutumia njia ya 'Promotion'. 


Post a Comment

0 Comments