REAL MADRID KUVUNJA REKODI YA DUNIA USAJILI WA MBAPPE.

Magwiji wa Hispania Real Madrid wanatarajia kuweka rekodi ya ulimwengu ya karibu € 400m ya kumsajili  nyota wa Ufaransa Kylian Mbappé kutoka Paris Saint-Germain, wakati tetesi zikieleza kuhusu hatma ya mshambuliaji huyo.

Mbappé amehusishwa sana na kuhamia Real Madrid ikiwa ni ndoto zake kuichezea kilabu hiyo. Pia amekuwa akivutiwa zaidi na magwiji hao wa Hispania.

Le Parisien sasa imeripoti (kama inavyonakiliwa na CalcioMercato.com) kwamba Madrid iko tayari kumletea nyota huyo mpya Santiago Bernabeu, kwa dau la € 400m ambayo inaelekea kuvunja  rekodi ya sasa ya usajili wa ulimwengu iliowekwa na Neymar kwa € 222m.

 Kwa ada iliyoripotiwa ni zaidi ya ada za hivi karibuni za Neymar na Cristiano Ronaldo.Mbappé amekua na mafanikio  PSG, ambao ni  mabingwa wa Ligue 1, pia akiwa na Ufaransa wamefanikiwa kubeba kombe la Dunia, hatua inayosababisha baadhi ya vilabu kuvutiwa na uchezaji wake.


PSG wameanza vizuri msimu mpya na Mbappé amekuwa akikadiliwa kuwa mchezaji ghali zaidi Duniani. PSG wako tayari kumuongeza mshahara nyota huyo ili abaki Ufaransa.

 Nyota huyo  amefunga mabao matano katika mechi zake saba za ligi hivi sasa, na tatu katika michezo mingine kwenye mashindano ya UEFA.Mabingwa hao wa Ufaransa wanatamani kushinda Ligi ya Mabingwa UEFA mwaka huu, na wameshinda katika mechi zao zote nne za kundi, wakipiwapiga Real Madrid

Post a Comment

0 Comments