SIMBA KUMUENGUA MMOJA KIKOSINI


Kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo msimu huu katika Ligi Kuu Bara inaelezwa kuwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba SC wanaweza kuachana na mchezaji mmoja kutoka Brazil.

Haijajulikana mpaka sasa ni nani ataachwa lakini tetesi zilizopo zinasema Wilker da Silva anaweza kuachwa kisha kusajiliwa mbadala wake.

Inaelezwa kuwa Simba hawajafurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo mpaka sasa kutokana na kushindwa kuonesha kile ambacho wengi wametarajia mpaka sasa.

Taarifa zilizopo zinasema wakati Kocha Mbelgiji, Patrick Aussema akisema anahitaji straika wa maana, Simba imelenga kusaka mchezaji huyo kutoka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Dirisha hilo la muda fupi litafunguliwa keshokutwa Novemba 15 tayari kwa timu kuanza usajili.


Post a Comment

0 Comments