SOMALIA: MWANAHARAKATI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Mwanaharakati wa Mashirika ya Kiraia nchini Somalia, Almaas Elman ameuawa kwa kupigwa risasi .

Tukio hilo lilitokea juzi  alipokuwa akisafiri kwa gari katika eneo lililopo karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu kuelekea nchini Kenya ambapo Wafanyakazi wengi wa Mashirika ya Kimataifa wanaishi

Almaas ambaye ni mtoto wa Mwanaharakati maarufu wa amani Nchini Somalia, Elman Ahmed aliyeuawa mwaka 1996, amefariki akiwa njiani kupeleka hospitali huku akiwa mjamzito

Alikuwa akirudi Somalia kusaidia Kituo cha kuwashawishi Watoto kuachana na makundi ya Silaha kilichoanzishwa na Mamake (Fartuun Adan) katika mipango yake ya kupambana dhidi ya unyanyasaji.

Post a Comment

0 Comments