BRAZIL: TIMU ILIYOPATA AJALI YA NDEGE YASHUKA DARAJA.


Klabu ya Chepecoense FC ya Brazil imeshuka daraja kutoka ligi kuu (Seria A) ikiwa ni miaka mitatu tangu timu hiyo kupata ajali ya ndege wakiwa wanaelekea nchini Colombia kwenye mchezo wa fainali ya Copa Sudamericana 2016.

Kipingo walichokipata siku ya Jumatano cha goli 1-0 kutoka kwa Botafogo kimewahakikishia kushuka daraja kutoka Serie A kwenda Serie B wakiwa wamebakiwa na mechi tatu mkononi, Chepecoense inashuka daraja ikiwa ni miaka sita tangu wapande kuingia ligi kuu.

Chepecoense ipo nafasi ya 19 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Brazil wakiwa na alama 28 huku Avai FC SC wakishika mkia kwa alama 18.

:TUJIKUMBUSHE
Novemba 29, 2016 Ndege iliyokuwa imebeba watu 81 wakiwemo maafisa na wachezaji wa timu ya Chepecoense FC ya nchini Brazil ilianguka wakati inakaribia mji wa Medellin nchini Colombia na kuua jumla ya watu 76 wakiwemo pia waandishi wa habari, msafara wote uliokuwa unaelekea kwenye mchezo wa fainali ya Kombe Copa Sudamericana dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya Colombia.

Post a Comment

0 Comments