Afisa wa Bodi ya Ligi Kuu asimamishwa kazi kwa kutoa taarifa za kukanganya katika mtanange wa Azam FC dhidi ya JKT Tanzania.


Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemsimamisha kazi kwa muda wa miezi miwili Afisa wake, Joel Barsidia baada ya kutoa taarifa ya kukanganya kuhusu mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL) kati ya Azam FC dhidi ya JKT Tanzania, uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Jumapili iliyopita.


Barsidia aliwaandikia barua Azam TV ambao ndio wanao rusha wa matangazo hayo kuwa mchezo utakuwa saa 10:00 jioni huku akiazindikia klabu (Azam na JKT Tanzania) kuwa mechi ni saa 1:00 usiku kabla ya kubadilisha tena.

Maamuzi hayo ya kumsimamisha Barsidia yametangazwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Steven Mguto huku akiiomba Azam radhi kwa tukio hilo ambalo lilileta mpasuko mkubwa.

"Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi ya ligi nichukue nafasi  kuiomba radhi Azam FC kwa mkanganyiko wa ratiba ambao umesabibiswa na Afisa wetu Joel Barisidia ambaye tumemsimamisha kazi kwa kosa hilo la uzembe," alisema Mguto.

Post a Comment

0 Comments