Atupwa jela miaka 30 kwa kumbaka bibi wa miaka 60


Mahakama wilayani Misungwi jijini Mwanza imemhukumu kwenda jela miaka thelathini (30) Bwana Shabo Marando (47), mkazi wa Kijiji cha Nange Mkoani Mwanza kwa kosa la kumbaka bibi wa miaka 60 .

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi na Esther Malick baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka uliokuwa na Mashahidi wanne.

Dkt Judith Kiwango kutoka hospitali ya wilaya ya Misungwi amesema baada ya kumfanyia uchunguzi bibi Huyo  alimkuta na michubuko sehemu za siri na manii nae shahidi wa pili upande wa mashtaka Sama Luheka amesema alisikia kelele kichakani aliposogea alimkuta mtuhumiwa huyo akimbaka bibi Huyo.

Nae bibi ambae ndiye mwathirika wa tukio hilo ameiambia Mahakama kuwa siku ya tukio Mtuhumiwa alimkuta shambani akikusanya kuni akamkamata kwa nguvu na kumvutia kichakani kisha kumbaka.


Post a Comment

0 Comments