Atupwa jela miaka miwili kwa kutishia kumuua Rais Magufuli.


Mahakama ya Mwanzo ya Ipembe mjini Singida, imemhukumu Bahati Martin (39), kifungo cha miaka miwili (02) kwenda jela kwa kosa la kutamka ya kwamba atamuua Rais John Magufuli

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutamka maneno hayo Novemba 26, 2019, huku siku ya pili yake (Novemba 27) Rais Magufuli na msafara wake ukipita Mkoani Singida kwenda Chato

Hakimu alitoa adhabu hiyo na kusema Mahakama imethibitisha pasi na chembe ya shaka kwamba mtuhumiwa alitishia kwa maneno hayo, kosa ambalo ni kinyume cha kifungu cha 89 (2) (9) sura ya 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu.


Mshtakiwa alitenda kosa hilo katika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi cha Zamani mjini Singida na baada ya kutamka maneno hayo, mara moja Raia Wema waliripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi na Askari walifika na kumtia mbaroni

Bahati alikiri kosa hilo lakini alijitetea kwamba alifanya hivyo akiwa na lengo la kutania tu wala hakuwa na lengo la kumuua Rais Magufuli.


Post a Comment

0 Comments