Aussems awapiga dongo viongozi wa klabu ya Simba

Aliyekuwa Kocha wa klabu ya Simba SC, Patrick Aussems amewaanga rasmi, Wachezaji na Mashabiki wa Simba na kusema kuwa bodi ya klabu hiyo ndio kikwaza kikubwa cha Mendeleo katika klabu ya Simba.


Aussems amesema kuwa kuendelea kwa klabu ya Simba kunatakiwa kuondolewa kwa baadhi ya viongozi ambao si wa kweli na wasio kuwa na elimu asa katika bodi ya wakurugezi ili kuwa na maendeleo katika klabu hiyo.

"Niwashukuru Wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya pamoja, Asante kwa Mashabiki kwa sapoti yenu. Kutoka ndani ya moyo wangu nawatakia kila la kheri! Nimshukuru Mo kwa kunileta katika nchini hii nzuri. Lakini ili kuendelea Simba inatakiwa kuondoka waongo na watu wasio na elimu katika bodi ambao ndio pingamizi kubwa katika Maendeleo ya klabu!"

"Hivi sasa ni wakati wangu wa kufurahia kitu cha muhimu katika maisha, Familia na watu wa kweli. Kwaheri Tanzania" alisema Aussems.


Post a Comment

0 Comments