AZAM FC KUANZA JALAMBA KESHO KUTETEA UBINGWA AZAM SPORTS FEDERATION.

Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), Azam FC, inatarajia kuanza kutetea taji hilo kwa kupambana na African Lyon kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya michuano hiyo utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex kati ya Desemba 22 na 23 mwaka huu.


Azam FC ilitwaa taji hilo msimu uliopita kwa kuichapa Lipuli ya Iringa bao 1-0, lililowekwa kimiani na mshambuliaji Obrey Chirwa na hatimaye timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Katika kujiandaa na mchezo huo, kikosi cha  Azam FC kitarejea kuanza mazoezini kesho Alhamisi jioni baada ya wachezaji kumaliza mapumziko ya siku tatu waliyopewa.


Post a Comment

0 Comments