Azam FC kukipiga dhidi ya Mtibwa Sugar katika kumbukizi ya marehemu Ibrahim Rajab "Jeba"..

Shirikisho la Soka visiwani Zanzibar (ZFA) limeandaa mchezo wa hisani kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Disemba 9 mwaka huu kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar, Saa 2:00 usiku, ili kuhenzi mchango wa kiungo aliyewahi kuzichezea timu hizo marehemu Ibrahim Rajab "Jeba" aliyefariki dunia Septemba mwaka huu.

Jeba aliwahi kucheza kwa mafanikio katika timu zote mbili (Azam na Mtibwa), Wakizungumzia mchezo huo viongozi wa timu zote mbili wamesema wamekubali kucheza mchezo huo ili kumuhenzi na kupata fedha kwa ajili ya kuichangia familia ya marehemu Jeba.

"Sisi kama Azam FC tumelipokea na tupo tayari kwenda kucheza mechi hiyo ili kupata fedha za kuweza kuchangia familia yake na ndugu zake wote. Tumeridhia na Tumekubaliana tayari" alisema Abdulkarim Amin, Mkurugenzi wa Azam FC.


"Tumekubaliana kucheza mchezo wa kumkubuka na kupata chochote kitu kwa familia amabayo inaitaji msaada. Marehemu Jeba alichezea timu zote mbili alikulia Azam na kuchezea Mtibwa alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa na kipaji kikubwa sana kama si maradhi na umati kumfika mapema alikuwa ni mchezaji anaonesha dalili za kufika mbali" Jamal Baysey, Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar.

Nae Katibu wa Bodi ya Ligi Kuu ya Zanzibar, Hussen Ahmada amesema wamechangua tarehe 9 kumuhenzi marehemu Jeba pamoja na tukio la sikukuu za  kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika.

Huku Afisa Habari wa Azam FC, Jafar Idd Maganga amesema katika mchezo huo siku hiyo kutakuwa na jezi maalumu za kumuhenzi marehemu Jeba, zitakazo kuwa zinauzwa kwa Mashabiki.


Post a Comment

0 Comments