Mbadala wa zahera atangaza kutua kwa kishindo yanga, ataka nauli na ya kutolea


Baada ya kuondoka kwa Mwinyi Zaheza siku za hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, amesema yuko tayari kutua Yanga.

Mexime amesema yeye ni Mwalimu wa mpira na mahala popote anaweza akaenda kama maslahi yanaweza yakiruhusu.

Akizungumza na Radio EFM kupitia kipindi cha E Sports, Mazime ameeleza kuwa Yanga bado hawajamtafuta lakini kama watakuja mezani na wakaelewana hataona tabu kuungana nao.Ameongeza kwa kusema yuko tayari endapo hata atahitajika kufanya kazi nyingine nje ya Ukocha Mkuu ilimradi waweze kuelewana malipo kama atayakubali.

"Mimi ni Kocha, mahala popte nafundisha.

"Yanga hawajazungumza na mimi, nitakuwa tayari kwenda kama wakishakubaliana nami juu ya maslahi nitakayohitaji.

"Hata leo naweza kutua Dar, kwa sasa nipo Morogoro, wanaweza tuma nauli pamoja na ya kutolea 'utani' ili nije tumalizane."
Post a Comment

0 Comments