Mfanyabiashara Marijan Msofe maarufu kam "Papaa Msofe" na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam wakikabiliwa na mashitaka matano ikiwemo utakatishaji wa fedha zaidi ya milioni 900.
Papaa Msofe sio mara yake ya kwanza kufikishwa mahakamani hapo kwani aliwahi kukabiliwa na kesi ya Mauaji mwaka 2012 kisha alifunguliwa kesi ya nyingine mnamo mwaka 2015.
Washitakiwa wengine ni Wakili wa Kujitegemea, Mwesigwa Mhingo,Fadhil Mganga, Wencelaus Mtui na Joseph Haule na miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni Kuratibu Genge la uhalifu,utakatishaji fedha na Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
0 Comments