Serikali hairidhishwi na mwenendo wa usajili wa vifo nchini

Licha ya kuwepo kwa faida nyingi za usajili wa vifo nchini,lakini kumekuwepo na mwamko mdogo wa wananchi kuona umuhimu wa zoezi hilo mara baada ya kifo.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi yao,idadi ya vifo nchini  vilivyosajiliwa inaonesha ni asilimia 17.5% tu ikiimaanisha vifo vingi haviandikishwi nchini.

Katika tathmini ya zoezi la usajili wa vifo mkoa wa Njombe lililofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe,waziri wa katiba na sheria balozi Augustine Mahiga amesema takwimu hizo haziridhishi na kuwataka watendaji kufanya jitihada za ziada ili kufikia malengo ya zoezi.


“Takwimu hizi haziridhishi kwa hiyo tufanye jitihada za ziada ili tuweze kufikia asilimia kubwa zaidi na ninaomba mikoa mingine ipate mfano wa Njombe kwasababu katika asilimia Njombe bado mnaongoza ukilinganisha na mikoa mingine”alisema Mahiga

Mahiga aliongeza kuwa ni muhimu kuandikisha na kupata cheti cha kifo mara vinapotokea ili kuweza kupata stahiki zinazomuhusu marehemu.

“Ni muhimu sana kuhakikisha tunaandikisha tukio hilo ili kupata vyeti vya kifo ambacho kinatumika kama uthibitisho wa kisheria na hutumiwa na familia na ndugu kupata stahiki mbali mbali zinazomuhusu marehemu,Ni muhimu sana kusajili vifo mara tu vinapotokea hata kama ni vya watoto waliozaliwa na kuishi kwa dakika chache”aliongeza Mahiga.


Post a Comment

0 Comments