Sumaye ajiengua CHADEMA ahidi kutojiunga na Chama chochote

Frederick Sumaye -Waziri Mkuu Mstaafu
Aliyewahi kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye (1995 hadi 2005) ametangaza rasmi kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwakile alichokisema ni baada ya kutafakari kwa kina na kuona wakubwa wamewashawishi watu wa Kanda ya Pwani kumpigia kura ya Hapana.

"Natangaza rasmi kujiondoa CHADEMA kwa sababu nimeshaonyeshwa sitakiwi, ninatoka CHADEMA ili kuondoa msongamano kwenye nafasi ya mwenyekiti taifa kulinda uhai wangu na sijiungi na chama chochote cha siasa ila niko tayari kutumika kama mshauri wa masuala ya siasa" amesema Frederick Sumaye


Frederick Sumaye ameutangaza uamuzi huo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo amedai kujiunga upinzani si jambo rahisi, kwamba alikuwa akiandamwa na Dola pamoja na familia yake.

"Kuhusu kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya CHADEMA, amesema, "Leo natangaza kuwa hiyo safari ya kugombea uenyekiti wa ngazi ya taifa naisitisha leo, kwa usalama wangu na familia kwa ujumla na Mbowe aliwahi kunitahadharisha kuwa sumu haionjwi kwa ulimi namimi sitaki kuionja"- amesema Sumaye.

Pia ametangaza kutokujiunga na chama chohote ila yupo tayari kutoa ushauri kwa chama chochote hata CHADEMA akihitajika.

"Mimi siyo mwanachama wa Chadema kuanzia sasa na sijiungi na chama kingine cha Siasa kuanzia leo na niko tayari kutumika katika chama chochote hata Chadema katika kushauri" amesema Frederick Sumaye.


Post a Comment

0 Comments