Kwanza nichukue nafasi
kusema asante ya hali ya juu
kwa wote walionitumia
salamu za heri kwa siku yangu
ya kuzaliwa kwenye ukuta
wangu wa FACEBOOK, hasa
wale walioandika HBD,
ambayo nimeambiwa ni kifupi
cha Handsome Boy of Dar es
Salaam umeona eee, ni wazi
hawa wana akili sana
wanastahili kupewa
ukurugenzi wa Bandari ya Dar
es Salaam, ntaongea na
Waziri husika, tukikutana
kwenye duka la kofia umeona
eee. Halafu sijui niongee
kingleza, maana asilimia 96 ya
mesej nilizopata leo ni za
kingleza. Zote zimeanza na
Happy Birthday, unaona ee,
which means asilimia 96 ya
marafiki zangu ni wazungu si
unaona ee. And then naona ni
wazungu kutoka nchi
mbalimbali, si unajua kwetu
Warusi , Wagiriki, Wataliano ,
Wamarikani, Waingereza na
kazalika wote ni wazungu,
umeona ee. Sasa nimegundua
kuwa nina marafiki wazungu
kutoka aina mbali mbali za
wazungu kutokana na jinsi
walivyomalizia ile Happy
Birthday, wengine wamesema
Happy Birthday Uncle,
wengine, Ankle, Ankali, Ankar,
Anko, Ango, Ankal umeona
eee. Hawa asilimia 4 ambao ni
waswahili wamenishangaza
sana, bila sababu za msingi
wameniita, Babu, Mzee,
Mkongwe, Veteran, why?
Nawapa siku saba waniombe
radhi aua nawapeleka
mahakamani na kuwadai
shilingi billion 300 kama fidia
umeona eeee, tusiharibiane
CV hivihivi live. Kuna wale
ambao bado naongea na
mwanasheria wangu ili kuona
hatua za kuwachukulia eti
wamenitumia picha za keki,
this is not for laugh, because
if forexambo I am try to eat
facebook, will you be happy?
Ehh sema will you be happy?
Zeafo tukutane tarehe kama
hii next yia of koz ntakuwa
nimelipwa fidia kutoka kwa
hawa waharibifu wa CV kwa
hiyo we will pariiiiiiiiiiiiii mpaka
deibrek auvipi??? Si umeona
eee
KWA HISANI YA JOHN KITIME