Mrembo Pendo Simon,ndiye aliyeshika taji la Redds Miss Mwanza 2012/13, ambapo aliwabwaga warembo 13 waliojitokeza kuwania taji hilo.
Shindano hilo lilifanyika Ijumaa ya wiki iliyopita katika viwanja vya Yatch Club Mwanza, ambapo mgeni Rasmi alikua ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga.
Shindano lilianza kwa burudani ya warembo kutoa show ya pamoja, ikifuatiwa na vazi la Ubunifu, Vazi la Ufukweni na Mwisho Vazi la Usiku la kutokea.
Warembo hao pia walipata fursa ya kuonyesha Vipaji vya aina mbalimbali.
Warembo waliongia Tano Bora na baadaye kuulizwa maswali ni pamoja na Happiness Daniel, Stella Augustino, Aisha Eddy, Clara Nuru na Pendo Simon.
Katika shindano hilo zawadi zilitolewa kama ifuatavyo
Mshindi wa Kwanza- 500,000/= na TV Inch 24
Mshindi wa Pili- 300,000/= na Decoder
Mshindi wa Tatu- 200,000/= na Decoder
Mshindi wa Nne- 100,000/=
Mshindi wa Tano- 100,000/=
Mshindi wa 6-13- 50,000/=
Wasani waliopanda jukwaani kutumbiza ni pamoja na Mwanahawa Ally katika miondoko ya Taarab, Bob Haisa na Jeeta Man kutoka Mwanza. Mwanamuziki Khadija kopa hakuonekana kwenye jukwaa na kuwaacha mashabiki vinywa wazi, ambapo alitangazwa kwamba angekuwepo. Baada ya kumuhoji Muandaaji wa shindano hilo, John Dotto juu ya kutokuwepo Khadija kopa, hata yeye alishangaa kutokuonekana malkia huyo wa Taarab, ambapo Dotto alidai tayari alishalipwa pesa yote ya Show Shilingi Milioni Moja. Dotto amesema walijaribu kuwasiliana naye kwenye simu ambapo malkia huyo alidai yuko njiani akitokea Kahama kuja Mwanza, tangu saa kumi na moja jioni siku ya tukio, hadi ilipofika saa 5 usiku hawakumuona mtu yeyote.
Inasikitisha kwa Mwanamuziki mkubwa kama huyo kuchukua pesa za watu halafu hatokei kwenye shughuli.
Hii haimaanishi kulidhalilisha shindano, hii inamaanisha kujidhalilisha yeye mwenyewe.aa