Bondia bingwa wa taifa wa kilo 59 toka
mkoa wa Tanga Said Mundi “smart punch”amefiwa na baba yake mzazi mzee
Abdulrahman mbaraka nyumbani kwake Zahrau mkoani Tanga.kifo hicho
kilitokea jioni ya jana muda mchache kabla ya mpira wa simba na yanga
haujaanza,sababu ya kifo chake cha ghafla inaelezwa ni shinikizo la damu
lilitokea kwa muda mfupi na kujaribu kumpeleka katika hospital bombo na
kufia njiani, kwa maelezo ya said mundi mwenyewe kwa Ibrahim
Kamwe”bigright” ni kuwa baba yake hapo awali hakuwa na ugonjwa huo
umekuja ghafla na umemchukua baba.
Wanategemea kuzika leo jioni.
Said Mundi anaetegemea kupanda ulingoni tarehe 26 octoba 2012 kuzichapa
na jumanne Mohamed raundi kumi kugombania ubingwa wa PST katika uwanja
wa mkwakwani-Tanga.viongozi wote wa masumbwi kwa pamoja tupo pamoja na
said mundi katika wakati huu mgumu uliompata na tunashirikiana katika
shughuli zima za kufanikisha msiba huu.Mungu ailaze roho ya mzee Abdi
Mbaraka mundi peponi – amin