Klabu ya Bongo Movie ambayo inaundwa na baadhi ya
wasanii wakubwa wa filamu nchini imepasuka katikati kisa kikidaiwa kuwa
ni lile tamko linalodaiwa kutolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Vincent
Kigosi ‘Ray’ kuwa mwanachama yeyote wa kundi hilo asitie miguu kwenye
msiba wa baba mzazi wa mwenzao, Wema Sepetu, marehemu Balozi Isaac
Sepetu.
Tukio hilo la katazo lilitokea wakati wa maombolezo ya kifo cha
mzee Sepetu kilichotokea Oktoba 27, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ
kwa ugonjwa wa kisukari ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwake, Sinza Mori
jijini Dar es Salaam.
Ray alaumiwa sana.
Kufuatia madai hayo, baadhi ya wasanii kutoka klabu ya Bongo
movies (majina tunayo) wamekuwa wakitoa lawama zao kwa Ray huku wengine
wakidai wamejitoa kwenye kundi hilo kwa sababu halina umoja na limejaa
unafiki.
Maneno hayo yalianza kusambaa baada ya Wema kumaliza kumzika baba yake Oktoba 31, mwaka huu mjini Zanzibar.
Wataka kumjadili
Habari za uhakika zinasema kwamba, wasanii waliotangaza
kujiengua klabuni humo wameshamuomba Ray aitishe kikao cha dharura kwa
ajili ya kuzungumzia hatua yake ya kuwapiga marufuku wasanii hao
kutoshiriki msiba wa mzee Sepetu huku akijua wema wa binadamu
unapatikana kwenye kushiriki mazishi ya wenzake.
“Kikubwa zaidi ni kwamba, Ray wakati akisambaza zile meseji
alisahau kuwa kuna siku Wema aliwahi kuwaalika wasanii wa kundi la Bongo
Muvi nyumbani kwake Makumbusho (Dar) wakala na kunywa, mbona hawakugoma
kwenda?” alihoji staa mmoja aliyepinga katazo la Ray.
Visingizio vya wanafiki “Tupa Kule”
Maumivu makali zaidi yaliibuka kufuatia baadhi ya wasanii
waliotaka kujifanya hawajapata meseji ya Ray ambapo walisema walishindwa
kushiriki msiba huo kwa sababu walikuwa ‘shooting’.
“Kuna wasanii walishindwa kuweka wazi kwamba walipokea meseji ya
katazo ya Ray, walipopigiwa simu na wenzao kuulizwa kwa nini
hawaonekani msibani kwa Wema walisingizia eti wako location wanarekodi!
“Kwa akili za kawaida, mwenzenu kafiwa mnaweza kushikwa na ubize
wa kurekodi filamu? Hawa ni wanafiki, walisingizia vile ili ionekane
wana hudhuru,” alisema staa mwingine.
Ray afunguka
Baada ya hayo yote hapo tuliamua kumfuatilia kwa karibu sana
mwigizaji vicent kigosi ili yujue kama madai haya ni ya kweli aua la na
haya ndo baadhi ya mambo aliyoweza kuyasema Ray.
“Kawaida yangu huwa sitetemeshwi wala kuyumbishwa na maneno
yamesemwa.mengi cna juu yangu lakini Mungu wa haki ananipigania….kweli
nimeamini ukubwa ni jalala na nyota yangu ni kubeba mizigo ya watu.
Mtasema sana Lakini Yangu Yananinyokea…” Alimaliza Ray.
Mmmh. Haya sasa mazito. Sisi yetu macho.
CREDITS; BONGO MOVIE.COM