Wachezaji
wa U17 wa Nigeria wakishangilia na kombe lao la dunia baada ya kuifunga
Mexico mabao 3-0 kwenye fainali iliyopigwa Uwanja wa Mohammad Bin
Zayed, Abu Dhabi jana.
Timu ya vijana waliochini ya miaka 17 (U17) wa Nigeria imetwaa
Kombe la Dunia kwa mara ya nne jana baada ya kuwalaza vijana waliochini
ya miaka 17 (U17) wa Mexico mabao 3-0 katika fainali iliyopigwa Abu
Dhabi. Pia Nigeria ilitwaa kombe hilo 1985, 1993 na 2007.