Msanii
wa filamu, Steve Nyerere amesema Wema Sepetu alikuwa hajitoi kwenye
matatazo ya wasanii wenzake wa filamu na ndio maana wasanii wengi wa
filamu wakashindwa kuhudhuria katika mazishi ya baba yake, Balozi Isaac
Abraham Sepetu mwishoni mwa mwezi uliopita.
Akizungumza
leo Steve,amesema anawataka watu waache kumtupia lawama Vicent Kigosi
aka ‘Ray’ wakati mwanadada huyo alikuwa hahudhurii katika matatizo ya
wenzake.
“Mnamlaumu
bure Ray jambo ambalo hajafanya kwakuwa Ray ni jalala basi kila kitu
mnamtupia,jamani mwacheni apumzike,” amesema Steve.
“Sisi
katika Bongo Movie Unity tuna uongozi, tuna mwenyekiti,tuna mwenyekiti
wa mipango ambaye ndio mimi, na tuna makamu wa mwenyekiti ambaye ndio
mimi na tuna makamu mwenyekiti ambaye ni Irene Uwoya. Lakini sisi
taratibu zetu kwenye misiba kama unaona kwenye misiba yetu
tunajitoa,lakini linavyotufika tunaangalia ni mwanachama gani naye
anakua anajitoa katika misiba ya wenzake