Yes ,Lovers!Once again,naleta mzigo mwingine muuthaminishe wenyewe…
Wote tuna mioyo
na hisia,wote tunafall in love kila siku maana tuko tunatafuta Penzi la
kweli…Penzi la kweli sometimes ni ngumu sana kulipata,ni safari yenye
milima na mabonde..the journey is hard…
Katika pitapita
yako,bahati nzuri ukaokota kijamaa au kidada,ukakipa moyo wako
mwenyewe,una-expect kitautendea haki…kitakupa mahaba..Kitakupa mambo
adimu,sio kama wale wengine ealioudundisha kama Kitenesi…
…..Kiupe mdomo wako smile na sio mnuno kama ufudu…
….Kiupe moyo wako sababu ya kupump damu kwa raha na sio kuuchezesha kiduku..
….Lakini wapi…Kinafanya tofauti na ulivyotegemea…
Inafikia kipindi
unaamua,bwana basi! Enough is enough wanasema Waingereza!Unanyosha
mikono juu hata kama unaamini wewe ni shujaa wa Mahaba..
Umejaribu kila mbinu kufanya Love Life yako ikupe furaha imeshindikana….
….Umejaribu kujifanya mjinga imeshindikana…
….Umejaribu kujitoa,kumfanyia mpenzi mambo mazito ambayo hata mzazi wako humfanyii maskini,Ili tu,Penzi lako liende vizuri….
LAKINI,Mtu
unayemfanyia hayo yote,Je,Yeye anachukulia mambo kwa uzito sawa na
wewe???Au umejitwisha Injini ya Scania peke yako???
Mara nyingi watu
tunaowapenda na kuwabeba mioyoni mwetu kwa uaminifu na Mapenzi na
Huba,hawajali lolote…Wanakuona Kichaa tu,na pengine
wanashangaa,kwanini huyu Mwanamke anahangaika hivi???Kwanini hili
Lijanaume linanipenda hivi,halina kazi???
TATIZO LINAPOKUJA,Pale unapoamua its over,utashangaa!!
Mtu huyuhuyu
aliyeonekana hajali lolote pamoja na Mapenzi yote uliyompa,anakuja kwa
nguvu,Atapiga magoti,ataomba marafiki msaada wamuombee msamaha…
Anaweza kuita
hata Matrafiki wamsaidie kukwamua gari lake
limenasa…Unajiuliza,alikuwa wapi hadi amesubiri haya yote yatokee ndio
aonyeshe umuhimu wako kwake kwa misamaha yenye ahadi kama nyingi kama
Ilani ya CCM??
ANAOMBA UMSAMEHE,UMPE NAFASI TENA…
Unaona sio ishu,maadam kaomba unampa…Anajitahidi wiki ya kwanza,fresh…Ya pili poa….ANASAHAU…
Mnarudi kulekule,vichozi vyako vilivyojikusanya kwa Wiki 2 za Mapenzi ya Ampicillin vinamwagika tena mwaaaaaaaaaaaaa…..
Na aliyevimwaga ni MTU YULEYULE??
Swali ni Je,NINI UMUHIMU WA SECOND CHANCE kwa mtu asiyeweza kuitumia Second Chance kujirekebisha????
Upuuzi uleule.
…Makosa yaleyale..
…Ujinga Uleule.
…Mateso yaleyale,na maskini ya Mungu Moyo ni huohuo,unauongezea tu Ufa….Matundu….Vidonda…..
JIHURUMIE WEWE KABLA HUJAMHURUMIA YEYE….
Kama kuumia unaumia wewe…Kama yeye alivyo na Moyo,na wewe unao pia,tena wa nyama….
Hata ukimpa SECOND CHANCES ELFU 8,kama habadiliki HAKUFAI…
Maana halisi ya
Second Chance huonekana pale MPEWA anapogundua Makosa na Udhaifu na
Kuitumia Second Chance kuonyesha kwamba Mapungufu yale ilikuwa ni Bahati
Mbaya tu na Kujisahau…..
Kumis-Use Second
Chance kwa Kurudia yaleyale ni TUSI kwako kwamba ”Wewe ni Mjinga kwa
kunipa Nafasi ya Kukuumiza kwa Mara nyingine tena”…
Think twice kabla hujampa Mtu Second Chance,ANAMAANISHA au Anaiomba kwa sababu ipo kwenye Kamusi????
TAFAKARI
CHANZO;http://www.sethought.blogspot.com