Na Shaffih Dauda
Mpira umemalizika Yanga 7-0 Wacomoro
Dakika ya 81, Didier Kavumbagu anaipatia Young Africans bao la saba
Dakika ya 75, Young Africans 6 – 0 Komorozine de Domoni
Dakika ya 68, Mrisho Ngasa anaipatia Young Africans bao la tano
Dakika ya 65, Mrisho Ngasa anaipatia Young Africans bao la tano
59′ Hamisi Kiiza anapigilia bao la nne…pasi nzuri ya Kavumbagu.
57′ Didier Kavumbagu anaipa Yanga bao la tatu.
54′ Komorozine wanapata mkwaju wa adhabu, Simba wanashangilia, Yanga wanazomea…bado mpira umesinzia.
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza,
Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Didier Kavumbagu kuchukua
nafasi ya David Luhende
HT: Yanga 2-0 Komorozine ( Ngassa, Nadir Haroub ) #CAFChampionsleague
42′ Yanga 2-0 Komorozine
39′ Hamisi Kiiza ana uchu mno wa kufunga, mpaka sasa offside mara nne,
32′ Komorozine wanapata kona ya kwanza. Kwa mara ya kwanza Simba wanapiga makofi.
Dakika ya 30, Young Africans 2 – 0 Komorozine de Domoni
23′ Timu nzima ya Komorozine imegeuka kwa mabeki. Hawavuki mstari wao.
20′ Nadir Haroub anamalizia kwa kichwa adhabu ndogo iliyopigwa na Msuva na kuaindikia Yanga bao la pili.
13′ Bao! Ngassa anachupa vizuri na kuiandikia Yanga bao la kwanza.
7′ Kisigino cha Hamisi Kiiza kinatua mikononi mwa kipa wa Komorozine.
2′ Kona tasa. Shuti la Ngassa lililokuwa likielekea nyavuni limepanguliwa na beki na kuwa kona. Krosi ya Msuva.
1′ Mpira umeanza…Yanga ndani ya jezi za kijani ilhali Komorozine wamevaa jezi za njano na bukta nyeusi.