Twiga
Stars imepoteza mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) baada ya leo kufungwa mabao
2-1 na Zambia (Shepolopolo) kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.

Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika katika mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga timu hizo zilikuwa suluhu.
Wenyeji
ndiyo walianza kupata bao lililofungwa na Hellen Mubanga dakika ya 75.
Mfungaji huyo aliyeingia kipindi cha pili nchini alimalizia wavuni mpira
uliotemwa na kipa Fatuma Omari.

Dakika
nne baadaye Zambia ambao walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu na washabiki
wao baada ya kufunga la kwanza, walipata bao la pili ambalo nahodha wa
Twiga Stars, Sophia Mwasikili alijifunga mwenyewe.

Mwasikili
alikuwa akijaribu kutoa nje mpira uliopigwa na nahodha wa Shepolopolo,
Mupopo Kabange ambapo ulipishana na kipa Fatuma Omari kabla ya kujaa
wavuni.

Bao
la Twiga Stars lilifungwa na Donisia Daniel dakika ya 90. Beki huyo wa
kushoto ambaye pia ni mchezaji wa Tanzanite alipanda mbele kuongeza
mashambulizi ambapo akiwa nje ya eneo la hatari alipiga shuti
lililomshinda kipa Hazel Nali.

Akizungumza
baada ya mechi, Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage alisema amebaini
upungufu katika kikosi chake ambao ataufanyia kazi kabla ya mechi ya
marudiano ili timu yake iweze kusonga mbele.

“Kwa matokeo haya bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano nyumbani na kusonga mbele,” alisema Kaijage.
Twiga
Stars iliwakilishwa na Fatuma Omari, Fatuma Bashiru, Donisia Daniel,
Fatuma Issa, Evelyn Sekikubo, Sophia Mwasikili, Vumilia Maarifa, Mwapewa
Mtumwa/Amina Ali, Asha Rashid, Etoe Mlenzi/Zena Khamis na Shelida
Boniface.

Timu
hiyo inarejea nyumbani kesho kwa ndege ya Fastjet ambapo itatua kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili
mchana.