Siku
chache kupitia mitandao ya kijamii mbalimbali kama Instagram,Facebook
na Twitter,Diamond Platnumz amekua akipost picha nyingi akiwaAfrika
kusini na wasanii mbalimbali akiwemo Dbanji.
Maswali yalikuwa mengi kichwani na mara nyingi tunaamini wasanii
wanapokutana pengine wana mipango ya kushirikiana kwenye kazi za kisanii
ama wana ukaribu mkubwa unaowafanya kuwa pamoja.
Millardayo.com imefatilia na kugundua safari ya Diamond South Africa
ni moja kati ya miradi ya One Campaign nah ii ya sasa ni kupitia mradi
wake wa Go Agric ambapo inahusu kufanya video na wimbo wa pamoja na
zaidi ya wasanii 20 wa Afrika.
Video tayari imefanyika Johannesburg Afrika Kusini kwenye studio za
M1 zinazomilikiwa na shirika la SABC,kwa Tanzania wasanii waliowakilisha
ni AY na Diamond,wasanii wengine waliopo kwenye mradi huo ni pamoja na
D’Banj,Femi Kuti wa Nigeria,Victoria Kimani wa Kenya na wengine.
Hizi ni pichaz wakati wanarekodi video ya wimbo huo.