MALOVEE? Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au ‘Mzee Mnyama’ na mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho THT’, wanadaiwa kuwa na uhusiano uliotafsiriwa ni wa kimapenzi, Ijumaa Wikienda limeinusa.
Mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho THT’
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali huku wakidaiwa kupiga ‘mitungi’ kiasi cha kushindwa kuzificha hisia zao.
Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au ‘Mzee Mnyama’.
“Mbona ipo wazi, TID na Recho siku hizi hawafichi kitu, tena wanapopiga mitungi ndiyo kabisa, mfano mzuri ni juzikati walikuwa pamoja mjini Dodoma, waliponda raha kinomanoma,” kilitiririka chanzo hicho.
Kama ilivyo ada, wanahabari wetu waliingia mzigoni kwa kuanzia nyumbani kwa Recho, Kinondoni, Dar, wakamkosa lakini badala yake, walipatikana mashosti zake wa karibu.
Kama ilivyo ada, wanahabari wetu waliingia mzigoni kwa kuanzia nyumbani kwa Recho, Kinondoni, Dar, wakamkosa lakini badala yake, walipatikana mashosti zake wa karibu.
“Recho kwa sasa anatoka na Mnyama na hapa tunavyoongea yupo Njombe ambapo ametimka baada ya taarifa za yeye kutoka na TID kuzagaa mtaani, halafu pia Recho siku hizi anapombeka sana na tunahisi hata ‘mambo meupe’ anatumia,” alisema shosti huyo.
Baada ya kushibishwa data hizo, waandishi wetu walitinga ofisini kwake THT, Kinondoni ambapo wanamuziki wenzake walisema staa huyo ana muda mrefu hajafika kazini hapo pasipo kutoa sababu za msingi.
Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Recho, akafunguka:
“Kweli nakunywa pombe lakini si kiivyo watu wanavyonisema. TID ni mtu wangu kikazi wala siyo kimapenzi. Watu wamekuwa wakinishutumu kila ninapokuwa na mwanaume wanasema ni bwana’ngu kitu ambacho si cha kweli kama wanavyonizushia kuvuta bangi.

“THT siendi kwa sababu nimesafiri, hapa ninapoongea nipo Njombe. Nimekuja kutulia huku kutokana na maneno kuzidi na watu kunipakazia uongo,” alisema Recho.
Kwa upande wake TID, alipopigiwa simu, alijitetea kwa kusema kuwa yupo na Recho kikazi na wala si vinginevyo.
“Dah…! Ebwana naomba uachane na hizo habari za mapenzi, mimi ni mtu mzima nina mengi ya maendeleo ambayo natakiwa nifanye,” alisema TID.