Rapper huyo alikiambia kipindi cha Sunrise cha Times FM kuwa wakati
Diamond anarekodi chorus hiyo yeye na Majani walishangaa kumuona
hitmaker huyo wa ‘My Number One’ akibubijikwa na machozi ndani ya
‘booth’.
“Lakini kilichotushangaza alipoingia booth ili arekodi chorus Diamond
alikuwa anaimba huku analia. Sisi tuko kwenye monitors huku
tunamuangalia jamaa upande wa pili kwenye booth tunamuona Diamond
analia. Alikuwa emotional unajua ile…ilimgusa sana. Sisi tulikuwa
tunashangaa mimi na Majani ‘huyu jamaa analia nini?’ Lakini baadae
tulimuuliza alituambia ‘nimefurahi sana katika maisha yangu kufanya kazi
na Profesa Jay pamoja na Majani, hilo moja. Lakini pili, mlivyoimba
humu ndani vyote vinanihusu mimi…vimenitokea sana katika maisha yangu na
changamoto zote hizo’..so yale ndio yalitokea studio. Kiukweli hii
ngoma ilikuwa blessed tangu studio na kila mtu alikuwa anasema ‘yeah men
it’s on’, alisema Profesa J.