Ni mwanaharakati wa muziki wa Hiphop ambaye mbali na kazi za kimuziki aliamua kujikita katika uwekezaji. Mwaka 2008 ndipo Andre Romelle Young, Dr. Dre wa sasa alianza shughuli zake za kutengeneza headphones akishirikiana na mjasiriamali mwenzake ambaye wako pamoja mpaka sasa,Jimmy Lovine wakiwa na kampuni yao inayoitwa Beats Electronics. Staa huyo wa kibao cha I need a Doctor amepata zali la kampuni yake ya Beats kukubalika kwa wamiliki wa kampuni ya Apple. Apple kampuni ambayo inajishughulisha na uzalishaji wa vifaa kama compyuta, simu na vinginevyo wako katika mazungumzo na Dr. Dre na Jimmy Lovine ili kufikia muafaka wa kuinunua kampuni ya Beats kwa kitita cha dola za Kimarekani billioni 3.2. Iko wazi kuwa baada ya kupokea kitita hiki wamiliki hao wawili watagawana na wadau wengi wa muziki wanakubali kuwa dili hili litamfanya Dre awe kileleni kwa wasanii wenye pesa nyingi. Apple wameripoti kuwa mchakato wa makubaliano utamalizika wiki ijayo.
Dre kwa sasa yuko nafasi ya pili katika listi ya wasanii matajiri Duniani kwa kuwa na dola milioni 500 huku nafasi ya kwanza ikikamatwa na P Didy mwenye mtonyo usiopungua dola za kimarekani milioni 700. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa mtandao wa Forbes.